Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza, Hujjat al-Islam wa al-Muslimin Sayyid Mohammad Reza Barqi alitangaza katika mkutano wa waandishi wa habari kuhusiana na kumbukumbu ya Ayatollah Golpaygani, akisema kwamba; hafla hiyo itafanyika siku ya Jumanne, 16 December, baada ya Swala ya Maghrib na Isha katika Msikiti Mkuu wa Qum Iran. Katika hafla hiyo, Hujjat al-Islam wa al-Muslimin Nasser Rafii atahutubia.
Misingi Mikuu ya Kumbukukizi hii:
Kama ilivyokuwa mwaka jana, misingi ya kumbukumbu hii itaangazia mada tatu kuu:
1. Shakhsia ya kielimu, fiqhi, na kijamii ya Ayatollah Golpaygani, ambaye alikuwa na mchango mkubwa katika historia ya Shia.
2. Uaminifu wa kipekee wa Marjii huyu mkubwa katika kuitumikia dini na watu.
3. Huduma zake endelevu ambazo zinaendelea hadi baada ya kufariki kwake.
Shakhsia Kubwa katika Hawza: Hujjat al-Islam wa al-Muslimin Barqi alisisitiza kuwa; Ayatollah al-‘dhzma Golpaygani alikuwa mtu wa historia, na alichukua nafasi muhimu katika maendeleo ya Hawza. Alikuwa mfuasi wa mfumo wa kielimu wa Ayatollah al-‘Udhma Sheikh Abdul Karim Haeri Yazdi (rahimahullah), na aliiongoza jamii ya Shia kama Marjii kwa zaidi ya miaka 35, na alitumia takriban miaka 85 ya maisha yake katika kufundisha na kutetea Elimu za Ahlul Bayt (as).
Mchango katika Uanzishwaji wa Taasisi za Kidini na Qur’ani: Hujjat al-Islam wa al-Muslimin Barqi alieleza kuwa uanzishwaji wa shule ya kwanza ya kielimu kwa mtindo mpya, pamoja na Dar al-Qur’an al-Karim ya kwanza, ni mojawapo ya michango muhimu ya Ayatollah Golpaygani, inayoonesha mtazamo wake wa kifasihi katika dini na tamaduni.
Kituo cha Kiislamu cha London:
Ayatollah al-‘udhma Golpaygani alianzisha Kituo cha Kiislamu kilichozungukwa na Waislamu wengi huko London, kilichokuwa na mchango muhimu katika kutoa mafundisho ya Ahlul Bayt (as) na kuwa mfano wa imara wa kuwepi Waislamu wa Shia huko Magharibi. Hujjat al-Islam wa al-Muslimin Barqi alieleza jinsi Kituo hicho kinavyofadhili matembezi ya Ashura kwa maelfu ya Waislamu, akionesha kiunganishi cha kihisia na kiitikadi cha Shia na tamaduni za Ashura.
Mfasiri wa Qur’ani katika Kumbukumbu ya Ayatollah Golpaygani:
Mwaka huu, shughuli za kumbukumbu zitazingatia muktadha wa sura ya marjii huyu kwa kutumia aya ya Qur’ani "إِنَّ الْأَبْرَارَ لَفِی نَعِیمٍ", ambapo wafasiri wa Qur’ani wanabainisha sifa tatu kuu za "abrar" (wale wema): Ukaribu wao na Mwenyezi Mungu, huduma zao kwa jamii, na kutokuwa na ubinafsi katika maisha yao—sifa hizi zote zilikuwa wazi katika maisha na utendaji wa Ayatollah Golpaygani.
Ushauri wa Kuhifadhi na Kutoa Urithi wa Wanazuoni Wakubwa:
Hujjat al-Islam wa al-Muslimin Barqi alisisitiza umuhimu wa kuhifadhi na kuhamasisha urithi wa wanazuoni na wahadhiri wakubwa katika jamii ya Kiislamu, na kusema kwamba kutumia vyema urithi huu kutaleta faida duniani na akhera. Aliongeza kwamba; juhudi za kushirikiana na taasisi za kiutamaduni na vyombo vya habari ni muhimu katika kuhamasisha na kueneza huduma za wanazuoni hawa katika vizazi vijavyo.
Maoni yako